Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandamano Kenya: Wanahabari sita wajeruhiwa katika visa tofauti

Maandamano Kenya: Wanahabari Sita Wajeruhiwa Katika Visa Tofauti Maandamano Kenya: Wanahabari sita wajeruhiwa katika visa tofauti

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Wanahabari 6 walijeruhiwa katika siku ya tatu ya maandamano dhidi ya serikali ya Kenya huku kukiwa na wasiwasi juu ya mashambulizi ya makusudi yaliyofanywa na serikali na waandamanaji dhidi ya vyombo vya habari.

Baraza la Habari la Kenya linasema wanahabari 25 wameshambuliwa tangu maandamano hayo kuanza wiki iliyopita.

Katika matukio ya Alhamisi, wanahabari 2 waliripotiwa kupata majeraha kutokana na vitoa machozi vilivyorushwa kwenye gari lao viungani mwa la jijini Nairobi.

Katika video ya kuogofya iliyoshirikiwa na kampuni ya uchunguzi ya Africa Uncensored, mtu aliyejifunika uso akiwa amevalia barakoa ya gesi anakaribia SUV nyeusi. Anaonekana kuvunja moja ya madirisha ya gari hilo kabla ya kurusha bomu la machozi.

Mwanamume aliyevalia shati la checked na suruali ya jeans ya buluu kisha anaondoka na kuungana na maafisa wa polisi waliovalia sar waliokuwa karibu na lori la maji ya mwasho.

Waandishi wawili wa habari wanasemekana kujeruhiwa katika tukio hilo, mmoja akiwa na majeraha makubwa kwenye shavu lake la kulia.

Huko Kisumu, mwanahabari mwingine alijeruhiwa vibaya alipokuwa akirekodi tukio la uporaji.

Taarifa ya Chama cha Wanahabari Kisumu inasema Bw Eric Nabiswa alirushiwa mawe na waporaji waliomwona akiwarekodi na kuanguka na kuvunjika baadhi ya mbavu alipoanguka akijaribu kutoroka.

Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya imelaani ongezeko la mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari wakiwa katika majukumu yao, ikiwa ni pamoja na wizi wa kutumia silaha na kulazimishwa kufuta picha za maandamano na polisi.

Wadau wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari na Chama cha Wahariri Kenya, wameitisha mkutano wa dharura wikendi hii ili kujadili ongezeko la chuki dhidi ya wanahabari katika machafuko yanayoendelea.

Chanzo: Bbc