Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandamano Kenya: Ulinzi mkali wa polisi washuhudiwa jijini Nairobi

Maandamano Kenya: Ulinzi Mkali Wa Polisi Washuhudiwa Jijini Nairobi Maandamano Kenya: Ulinzi mkali wa polisi washuhudiwa jijini Nairobi

Tue, 2 May 2023 Chanzo: Bbc

Idadi kubwa ya polisi wamesambazwa katika maeneo mbali mbali yam ji mkuu wa Kenya Nairobi kabla ya kufufuliwa kwa maandamano ya Muungano wa upinzani wa Azimio la Umoja dhidi ya serikali .

Polisi wamewekwa kwenye maeneo makuu ya kuingia katika jiji la Nairobi na kutoka, ikiwa ni pamoja na barabara za Uhuru -Uhuru Highway - Haile mtaa wa Selassie, na baadhi ya maeneoya Ngara, na karibu na G.P.O.

Hali hiyo pia imeshuhudiwa katika barabara ya Ngong.

Vizuizi pia vimewekwa katika barabara inayoelekea katika ofisi za Ikulu , huku maafisa wa polisi wakionekana katika barabara zinazoelekea kwenye Ikulu hiyo.

Katika baadhi ya meneo yam ji wa Kisumu ambao ni ngome ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga, tayari maandamani yamekwishaanza huku waandamanaji wakiripotiwa kufunga barabara kwa mawe na kuwasha moto barabarani.

Katika taarifa aliyoitoa kuhusu maandamano ya Muungano wa Azimio la Umoja, Kamanda mkuu wa polisi kanda ya NairobiAdamson Bungei alidai kuwa Azimio hawakuonyesha kuwa na malengo mazuri katika maandamano yao yaliyopita, akasema hawafai kuongoza maandamano.

Kwa upande wake, Rais William Ruto aliapa kutumia mamlaka yote aliyonayo kuhakikisha kuwa maandamano yaliyopangwa hayageuki kuwa vurugu na ghasia.

Hata hivyo kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga ameapa kuwa maandamano lazima yaendelee kwani anasema serikali ya Rais Ruto haiku tayari kushughulikia masuala, mkiwemo kushugulikia gharama za maisha, kufunga seva za matokeo ya uchaguzi, kufanyika kwa mageuzi katika utendaji wa Tume ya uchaguzi.

Chanzo: Bbc