Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandamano Kenya: Polisi wawakabili waandamanaji

Maandamano Kenya: Polisi Wawakabili Waandamanaji Maandamano Kenya: Polisi wawakabili waandamanaji

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Maandamano ya siku tatu yaliyotishwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga akiwataka wafuasi wake kujitokeza na kuandamana ili kupinga gharama ya juu ya maisha yameanza katika maeneo tofauti nchini Kenya.

Tayari makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa polisi yameanza kushuhudiwa katika eneo la kibra mjini Nairobi ambapo maafisa wa polisi wamelazimika kutumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji.

Mjini Mombasa maafisa wa polisi walimkamata mtu mmoja mapema leo baada ya waandamanaji kuwasha matairi barabarani na kufunga barabara inayoelekea katika bandari ya kenya.

Vilevile polisi katika maeneo ya mji wa Nakuru eneo la Shabab wanajaribu kuwazuia vijana ambao wamejitokeza barabarani kufanya maandamano.Hatahivyo maafisa wa polisi waliwarushia vitoa machozi na kuwatawanya.

Mjini Eldoret ambako ni nyumbani kwa rais William Ruto hali ipo shwari na wakazi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.

Katika maeneo ya mkoa wa kati , hakuna visa vya utovu wa nidhamu vilivyoripotiwa, ijapokuwa kuna idadi kubwa ya polisi waliopelekwa katika maeneo ya biashara kuhakikisha kuwa usalama unaimarishwa

Mjini Kisumu, waandamanaji waliwasha matairi huku maandamano yakianza. Hatahivyo kumekuwa na idadi kubwa ya maafisa wa polisi waliopelekewa katika maeneo tofauti ya nchi ili kuimarisha usalama.

Wakati huohuo baadhi ya miji mikuu nchini Kenya iliendelea kusalia kuwa mahame katika kipindi cha alfajiri – huku Maandamano hayo yakianzishwa.

Chanzo: Bbc