Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amewaambia raia kwamba haki zao za kuandamana "hazimpi yeyote haki ya kunyanyasa, kutisha au kumtishia mtu yeyote".
Pia ameonya dhidi ya uharibifu wa mali au kuwadhuru watu wengine.
Hii inakuja huku maandamano yakifanyika maandamano yaliyoandaliwa na kikuu cha chama cha upinzani cha- Economic Freedom Fighters (EFF) yakifanyika kote nchini humo.
Maandamano hayo yaliyopewa mada ya -usimamishwaji wa shughuliza kitaifa, waandamanaji wanamtolea wito Rais Cyril Ramaphosa n kujiuzulukwakimshutumu kwa ufisadi na kushindwa kushughulikia mzozo wa nishati.
Hadi sasa polisi wa Afrika Kusini wamewakamata watu 87 kuhusiana na maandamano. Serikali pia imewaweka zaidi ya wanajeshi 3,000 kusaidia kulinda miundo mbinu.
"Kama vile taifa lina jukumu la kuuunga mkono haki ya maandamano ya amani, lina wajibu pia wa kuzuia jaribio lolote la kukiuka haki yoyote ya kikatiba.’’ Rais alisema katika taarifa.