Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maambukizi ya virusi vya COVID-19 yazidi kupungua, wizara ya Afya yatangaza

Efc3cc61272190d0 Maambukizi ya virusi vya COVID-19 yazidi kupungua, wizara ya Afya yatangaza

Tue, 20 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Watu wengine 241 wamepatikana na virusi vya COVID-19 baada ya sampo 2, 515 kufanyiwa vipimo chini ya saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa asilimia ya maambukizi imepungua hadi 1.9% kutoka 22 % tangu wakati Rais Uhuru Kenyatta alipotangaza kafyu kwa kaunti tano ikiwemo Nairobi, Kiambu, Kajiado, Machakos na Nakuru.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya, jumla ya idadi ya maambukizi ya virusi vya COVID-19 kwa sasa imefikia 151, 894 na sampo zilizopimwa zimefikia 1,605,847 kwa jumla.

Kati ya visa vilivyoripotiwa Jumatatu, Aprili 19, 228 ni Wakenya ilhali 13 ni raia wa nchini za kigeni, 135 ni wanaume na 106 ni wanawake, mgonjwa wa umri mdogo ana miaka 13 huku wa mkubwa ana miaka 90.

Hata hivyo, watu wengine 20 wamepoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo na kupelekea idadi ya vifo nchini kufikia 2,501.

Wagonjwa 636 wamepona kutokana na ugonjwa huo , 487 walikuwa wakipokea matibabu wakiwa wametengwa manyumbani huku 149 wakiruhusuwa kuondoka katik hospitali mbali mbami nchini.

Wagonjwa waliopona kutokana na ugonjwa huo kwa sasa ni 102,278, huku 1,651 wakiwa wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya na 6, 161 wakiwa wametengwa nyumbani waki chini ya uangalizi wa kimatibabu.

Kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya, wagonjwa 250 wamo katika vyumba vya ICU, 57 wamewekwa kwenye ventileta, 150 wanatumia oksijeni na 43 wako chini ya uangalizi wa madaktari.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690

Tazama habari zaidi hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke