Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maajabu, Sampuli kutoka Shule ya Upili ya Eregi kutoonesha ugojwa- KEMRI

Maajabu, Sampuli Kutoka Shule Ya Upili Ya Eregi Kutoonesha Ugojwa  KEMRI Maajabu, Sampuli kutoka Shule ya Upili ya Eregi kutoonesha ugojwa- KEMRI

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matokeo ya sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Eregi yametangazwa hadharani.

Sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa wasichana hao na Taasisi ya Utafiti ya Matibabu ya Kenya (KEMRI) zinaonyesha kuwa wanafunzi hao hawa na ugonjwa wowote.

Mkurugenzi Mkuu wa Afya Kaunti ya Kakamega Bernard Wasonga alifichua hilo.

"Hakukuwa na maambukizi hata kidogo kutokana na hali zao, KEMRI imeleta matokeo ya sampuli zilizochukuliwa na yanaonyesha hakuna ugonjwa," alisema.

Matokeo ya sampuli yalitoka kwa angalau wanafunzi 44 kati ya wanafunzi 106 wanaougua ugonjwa huo wa ajabu.

Wale wamebaki ni 62, wataendelea na masomo yao bila shida yoyote. Wanafunzi hao wanasemekana bado wanaonyesha dalili za miguu dhaifu na ugumu wa kutembea.

Kisa hicho cha ajabu kiliwaacha wanafunzi wengine shuleni wakiwa na wasiwasi huku wanafunzi wakitaka waruhusiwe kwenda nyumbani na wazazi wao.

Shule hiyo baadaye ilifungwa kwa muda siku ya Jumatano na inatazamiwa kufunguliwa tena wiki ijayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live