Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maafisa wa polisi waokoa maisha ya mtoto aliyezaliwa bafuni

B33a0133f3786c46 Maafisa wa polisi waokoa maisha ya mtoto aliyezaliwa bafuni

Wed, 14 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mtoto huyo yuko buheri wa afya baada ya juhudi za polisi kufanikiwa

- Baba ya mtoto huyo alisema alikuwa ameanza kujiandaa kumpeleka mke wake hospitalini lakini alipata uchungu wa uzazi ghafla

- Alizaliwa vyema lakini alihitaji msaada wa madaktari kwa sababu ya kushindwa kupumua

Mtoto Nico alizaliwa bafuni katika jimbo la New Jersey siku ya Ijumaa Kuu mwendo wa saa nane unusu asubuhi.

Baba ya mtoto huyo alisema alikuwa ameanza kujiandaa kumpeleka mke wake hospitalini lakini alipata uchungu wa uzazi ghafla.

Nico alizaliwa vyema lakini alihitaji msaada wa madaktari kwa sababu ya kushindwa kupumua.

"Kichwa nilisukuma mwenyewe. Lakini mwili mzima nashukuru mume wangu alikuwepo kusaidia," alisema mama Sasha Jackson.

Wakati maafisa Mueller na Rob Cangialosi waliwasili, bado mtoto huyo alikuwa kimya na ngpzi ya bluu, wakamfunga na blanketi wakitafuta mizizi yake.

"Walimuomba mwenzagu sirinji. Dakika chache baadaye, rangi ya ngozi yake ilianza kubadilika," alisema afisa wa Kituo cha Polisi cha Wood-Ridge Mike Mueller.

Kando na kumsaidia mtoto huyo kupumua, walitumia kamba ya viatu ya baba yake kukata kitovu chake.

Maafisa hao pia walirejea na kumupa Nico sare ya polisi na kaka yake mkubwa Luca akipokea gari la polisi la watoto kuchezea.

"Bora familia ina afya, ni siku njema kwetu," Cangialosi alisema.

Familia ya Jacksons wanafurahia kuwa na watoto wawili wa kiume wenye afya.

Maafisa hao wawili sasa wana watoto wawili wa kimu, na hawatasau namna Nico aliwasili mapema.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke