Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maafisa wa jeshi wamtembelea 'Yesu wa Tongaren'

Yesu Tongaren Kutembelewa.png Maafisa wa jeshi wamtembelea 'Yesu wa Tongaren'

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) wamemtembelea kiongozi huyo wa kiroho wa Kanisa la New Jerusalem Sect, Eliud Simiyu maarufu ‘Yesu wa Tongaren’ anayeishi Kaunti ya Bungoma ambaye anajinasibu yeye ni Yesu ambaye yupo kwenye mchakato wa kuiokoa Dunia.

Kumekuwa na Wakenya wengi wanaomtembelea na wengine kumkosoa baada ya mtumishi huyo kuripoti katika vyombo vya usalama akidai waumini wake wanataka asulubiwe katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka kama ilivyokuwa kwa Yesu

Maofisa hao walipiga picha na Yesu wa Tongaren, kitendo hicho kimepokelewa kwa mitazamo tofauti kwenye mitandao ya kijamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live