Ndege ya shirika la Umoja wa Mataifa (UN) imepigwa na kuangushwa nchini Sudan katika vita na machafuko yanayozidi kushuhudiwa nchini humo.
Ndege hiyo ya shirika la UN kitengo cha kusambaza chakula duniani (WFP) imedunguliwa ikiwa na maafisa wake wa kusambaza chakula ambao wameaga dunia.
“Nimeshtuka na kuhuzunika kwa mauaji ya wafanyakazi watatu wa shirika la WFP yaliyotokea Jumamosi - Aprili 15 - katika machafuko eneo la Kabkabiya, Darfur Kaskazini wakati wa kutekeleza majukumu ya kuoa maisha kwa kukabili baa la njaa ulimwenguni," amesema Cindy McCain, Afisa Mkuu Mtendaji wa WFP.
Kwa tukio hilo, WFP sasa imetangaza kusitisha oparesheni zake zote za kutoa msaada nchini Sudan, kwani maisha ya maafisa wao yana umuhimu mkubwa.