Wed, 9 Feb 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Maafisa nchini Uganda wanataka ipitishwe sheria ya kuifanya chanjo kuwa kitu cha lazima nchini humo.
Muswaada huo unalenga kuhamasisha watu zaidi kujitokeza kuchoma chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Aidha sheria hiyo inayopendekezwa inataka mtu kuchukuliwa hatua ya kufungwa jela hadi miezi sita endapo atakataa kupokea chanjo hiyo.
Waziri wa afya wa Uganda mnamo mwezi uliopita alisema zaidi ya chanjo 400,000 ziliharibiwa baada ya muda wao kumalizika bila ya kutumika.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live