Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maafisa 27 Kenya wasimamishwa kazi kuruhusu sukari iliyokwisha muda

Maafisa 27 Kenya Wasimamishwa Kazi Kuruhusu Sukari Iliyokwisha Muda Maafisa 27 Kenya wasimamishwa kazi kuruhusu sukari iliyokwisha muda

Thu, 18 May 2023 Chanzo: Bbc

Serikali imewasimamisha kazi maafisa 27 kutoka taasisi kumi na mbili waliosaidia kuachiliwa kwa sukari iliyokwisha muda wake ambayo ilikuwa imepangwa kuharibiwa mwaka wa 2018, hatua ambayo ilihatarisha wananchi ambao huenda walinunua bidhaa hiyo.

Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei Jumatano alitangaza kwamba kusimamishwa kazi kumechochewa na wizara mbili - Hazina ya Kitaifa inayoongozwa na Njuguna Ndung'u na Uwekezaji na Biashara inayoongozwa na Moses Kuria - ikisubiri kukamilika kwa uchunguzi wa kisa hicho.

Shirika la Viwango vya bidhaa nchini Kenya (Kebs) lilikuwa limeona kuwa mifuko 20,000 ya sukari haifai kwa matumizi ya binadamu na ikaagiza ibadilishwe kuwa ethanoli ya viwandani.

Lakini shehena hiyo badala yake iliingizwa sokoni kinyume na sheria .

"Ubadilishaji wa ethanoli ya viwandani ulipaswa kutekelezwa chini ya usimamizi wa pamoja wa mashirika ya Kebs na Nema chini ya mfumo wa mashirika mengi. Tangu wakati huo imethibitishwa kuwa shehena hiyo ilielekezwa kinyume na utaratibu na kutolewa bila utaratibu. Zaidi ya hayo, masharti yanayohusiana na uandikishaji wa wazi na wa ushindani wa bidhaa hiyo yalikiukwa na ushuru uliohitajika haukulipwa,” Bw Koskei alisema kwenye taarifa.

Taasisi ambazo maafisa wao wamesimamishwa kazi ni Kebs, Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA), Huduma ya Kitaifa ya Polisi, Afisi ya Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai (DCI), Mamlaka ya Kilimo na Chakula (AFA), Huduma za Afya Bandarini.

Chanzo: Bbc