Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maafisa 2 waliompiga risasi mwanamke 2018 wapatikana na hatia ya mauaji

25c0c7e89339e698 Maafisa 2 waliompiga risasi mwanamke 2018 wapatikana na hatia ya mauaji

Wed, 12 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mahakama Kuu ilimpata polisi Konstebo William Chirchir na Godfrey Kirui na hatia ya mauaji ya mfanyabiashara Jane Wangui Waiyaki

- Maafisa hao wawili walimpiga risasi mwanamke huyo mnamo Mei 2018 wakati alikuwa ndani ya gari lake na mpwa wake Bernard Chege ambaye alipata majeraha mabaya

- Jaji Stella Mutuku alisema wawili hao walikuwa na nia ya kumuua mwanamke huyo licha yake kutokuwa tishio kwa usalama.

Maafisa wawili wa polisi waliompiga risasi mfanyabiashara Jane Waiyaki mnamo Mei 2018 wamepatikana na hatia ya mauaji.

Konstebo William Chirchir na Godfrey Kirui walimpiga risasi mwanamke huyo na mpwa wake Bernand Chege walipokuwa wakipumzika kwenye gari lake asubuhi ya Mei 20, 2018.

Wakati akitoa uamuzi huo Jumanne, Mei 11, Jaji wa Mahakama Kuu Stella Mutuku alisema maafisa hao wawili walitumia nguvu kupita kiasi licha ya mwathiriwa na mpwa wake kutokuwa tishio kwa usalama.

Mutuku alisema wawili hao pia hawakuwa wamefanya uhalifu wowote wakati maafisa hao waliwafyatulia risasi wakinuia kuwaua.

Pia alisema kuwa maafisa hao hawakufyatua risasi hewani kuwatisha lakini badala yake walipiga risasi moja kwa moja kwenye kiti cha abiria.

"Maafisa wote walikuwa na silaha, na walipaswa kuchukua tahadhari. Ninaamini kulikuwa na njia zingine za kusimamisha gari hilo, na pia walikiuka sheria inayowataka kulinda maisha," alisema katika uamuzi huo.

Kulingana na maafisa wa usalama gari hilo lililokuwa na vioo vya rangi nyeusi liliripotiwa kuonekana likiwa limeegeshwa kenye bustani hiyo.

Maafisa wa polisi wa Makadara ambao walikuwa wamshika doria walibisha kwenye dirisha la gari hilo lakini hamna yeyote aliyewajibu.

Ripoti hiyo ilionyesha kuwa gari hilo liliondoka kwa kasi na kusababisha maafisa hao wawili kufyatua risasi 11 ndani ya gari.

Kijana huyo wa miaka 41 na mpwa wake wa miaka 26 walipatikana ndani ya gari hilo wakiwa uchi huku mama huyo akiaga dunia kutokana na majeraha ya riasi naye mpwa wake akiachwa na majeraha mabaya.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke