Leo bara la Afrika linaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), unaojulikana sasa kama Umoja wa Afrika (AU), ulioanzishwa rasmi Mei 25, 1963, mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia.
AU inaadhimisha Siku hiyo chini ya kauli mbiu: "Afrika Yetu Mustakabali Wetu" kwa kutumia alama ya reli #OurAfricaOurFuture. Shughuli za kuadhimisha za kihistoria zitafanyika katika bara zima la Afrika na nchi 55 wanachama wa AU.
Nchi zote wanachama zinatarajiwa miongoni mwa mambo mengine kuonyesha mafanikio makubwa, hatua muhimu, changamoto, na njia ya kusonga mbele chini ya Ajenda ya 2063.
Katika taarifa yake, AU imesema inaadhimisha Siku ya Afrika, kwa kutambua dira na hatua muhimu iliyofikiwa kuelekea Afrika iliyounganishwa, yenye ustawi na amani, inayoendeshwa na raia wake yenyewe na kuwakilisha nguvu mahiri katika nyanja ya kimataifa.
"Hii, kwa kuwakumbuka wanachama wake waanzilishi, ambao ndoto yao ilikuwa kujitahidi kwa Afrika iliyoungana, yenye amani na yenye kuwakilisha nguvu mahiri katika medani ya dunia na zaidi hasa, mapambano dhidi ya ukoloni. Hatimaye, nchi nyingi za Afrika zilipata uhuru katika miaka ya 50 hadi 60 na baadaye miaka ya 90 kwa vita dhidi ya ubaguzi wa ra