Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MTN Afrika Kusini Kuzindua Huduma za 5G

MTN.jpeg MTN Afrika Kusini Kuzindua Huduma za 5G

Tue, 30 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya huduma za mawasiliano Afrika Kusini ya MTN imetangaza kuwa itazindua huduma za teknolojia ya 5G nchini huko kuanzia Juni 30, 2020. Kampuni hiyo imepanga kufanya uzinduzi huo kwa kutumia idhaa yake ya YouTube kutokana na hali ya janga la Corona katika taifa hilo.

MTN imetangaza kuwa kutakuwa na huduma ya mtandao yenye kasi ya hali ya juu katika majiji makubwa ambayo majina yake yatatangazwa wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.

Hapo mwanzoni, kampuni hiyo ilikusudia kuzindua huduma hiyo mapema mwezi juni lakini ilikumbana na changamoto na kuchelewa kwa baadhi ya vifaa katika nchi hiyo, Shirika la habari la Business Insider liliripoti.

Huduma hii ya MTN inakuja miezi miwili baada ya mshindani wake, kampuni ya Vodacom Afrika Kusini kuzindua 5G tangu tarehe 4 Mei 2020 katika majiji matatu ya Johannersburg, Preitoria na Cape Town, na kutangaza kuwa itaanza kufikisha huduma hiyo sehemu mbalimbali ya taifa hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live