Maelfu ya wakimbizi wa Sudan mashariki mwa Chad huenda "wakakwama na kusahaulika" msimu wa mvua unapoanza, shirika la misaada la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) linasema.
Maeneo yanayokaliwa na wakimbizihuenda yakatengwa, kwani mito inajaa maji na kufurika katika eneo linalozunguka, kulingana na MSF.
Ghasia za hivi majuzi nchini Sudan zimefanya zaidi ya watu 100,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, kukimbilia nchi jirani ya Chad.
Baadhi yao wanaishi katika maeneo ambayo tayari yana idadi kubwa ya wakimbizi na yanaathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
"Tunakabiliwa na mzozo juu ya nyingine," shirika la misaada lilisema katika taarifa.
Linaongeza kuwa watu huenda wakaamua kurejea Sudan kukabiliana na ghasia zaidi huku hali nchini Chad ikizidi kuwa mbaya.
MSF imetoa wito wa kuongezwa kwa juhudi za kimataifa za kushughulikia hali nchini Chad.