Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MPOX: Kenya yathibitisha kesi ya kwanza ya maambukizi

Monkey Pox MPOX: Kenya yathibitisha kesi ya kwanza ya maambukizi

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kenya imethibitisha kisa cha kwanza cha maradhi ya homa ya nyani maarufu Mpox katika eneo la kusini-mashariki mwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Virusi hivyo viligunduliwa kwa mtu aliyekuwa akisafiri kutoka Uganda hadi Rwanda kupitia Kenya.

Wizara ya Afya ya Kenya inasema msongamano mkubwa wa watu kati ya Kenya na mataifa mengine ya Afrika Mashariki unaleta hatari kubwa ya kuenea kwa ugonjwa huo katika eneo hilo.

Kupitia katibu wa wizara ya afya Mary Muthoni Muriuki, wizara hiyo imesema kuwa inashirikiana na serikali za Kaunti ili kuhakikisha kuwa maradhi hayo yanazuiwa haraka iwezekanavyo.

Wasiwasi unaongezeka kuhusu kuenea kwa aina mpya na hatari ya maradhi hayo katika eneo la Afrika Mashariki.

Maambukizi mengine ya ugonjwa huo pia yameripotiwa katika mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Homa ya nyani, ambayo zamani ilijulikana kama monkeypox ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya monkeypox.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live