Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MONUSCO yamaliza operesheni zake Kivu Kusini

Vikosi UN Na Drc.jpeg MONUSCO yamaliza operesheni zake katika mkoa wa Kivu Kusini

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO), wamemaliza rasmi operesheni zao katika mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa nchi, baada ya miaka 20.

Kwa mujibu wa mipango yao, MONUSCO ilikuwa ifunge shughuli zake katika mkoa huo kuanzia tarehe 1 mwezi Mei.

Baada ya kuondoka Kivu Kusini, walinda amani amani hao wataendelea na operehseni zao katika mkoa wa Kivu Kaskazini na Ituri, wakati huu wakiwa na mpango wa kuondoka kabisa nchini humo kufikia mwisho wa mwaka huu.

Hivi karibuni msemaji wa MONUSCO Luteni Kanali Kedagni Menhsah alisema MONUSCO kwa upande wake imejizatiti kutekeleza mamlaka mpya iliyopatiwa kuhusu awamu za kuondoka DRC, huku ikiruhusu jeshi la kitaifa la ulinzi na usalama kurejea kwenye majukumu yake kwa kujitegemea.

Kituo cha MONUSCO cha Kamanyola, huko Kivu Kusini ambacho kilikuwa kinatumiwa na walinda amani hao wa Umoja wa Mataifa kutoka Pakistani kilifungwa tarehe 28 mwezi Februari mwaka huu na majengo yake kukabidhiwa ka Polisi wa kitaifa nchini humo, CNP.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live