Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MONUSCO kuanza kuondoka nchini DR Congo

DRC Yadai Rwanda Inafadhili Waasi Wa M23 MONUSCO kuanza kuondoka nchini DR Congo

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Mataifa unatarajiwa kuanza mchakato wa kuwaondoa wanalinda amani wake MONUSCO nchini DR Congo kwa kukabidhi kwanza moja ya kambi zake kwa polisi wa kitaifa.

DRC iliwataka wanajeshi hao kuondoka licha ya UN kuelezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la usalama mashariki mwa taifa hilo.

Kinshasa inasema walinda amani wa Umoja wa Mataifa wameshindwa na jukumu lao la kuwalinda raia dhidi ya mashambulio ya makundi ya watu wenye silaha mashariki mwa taifa hilo.

Baraza la usalama katika UN mwezi Desemba mwaka uliopita, lilipiga kura kuridhia ombi la Kinshasa la kutaka kuondolewa wa wanajeshi MONUSCO kwa awamu.

Ujumbe wa MONUSCO uliwasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka wa 1999.

Kikosi hicho kwa sasa kina wanajeshi karibia 13,500 na polisi 2,000 mashariki wa nchi hiyo haswa katika miji ya Ituri, Kivu Kusini na Kivu Kaskazini.

Mpango huo wa kuondoka kwa MONUSCO unatarajiwa kutekelezwa kwa awamu tatu, ambapo kambi ya kwanza kuwasilishwa kwa mamlaka ya DRC ni ile ya Kamanyola, kwenye mpaka na nchi ya Burundi.

Wanajeshi walio katika maeneo ya Kivu Kusini ndio wanaotarajiwa kuondoka katika awamu ya kwanza kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili na baadae kufuwatiwa na wafanyikazi raia kwenye eneo hilo tarehe 30 ya mwezi Juni.

Kabla ya mwezi Mei, Umoja wa Mataifa unatarajiwa kuwa umeondoka kwenye kambi 14 kwenye majimbo husika na kuzipeana kwa maofisa wa serikali ya DRC.

Hatua ya kuondoka kwa walinda amani hao wa UN inakuja wakati huu mapigano yakiendelea kuripotiwa katika eneo la Kivu Kaskazini kati ya jeshi la DRC na waasi wa M23.

Mapigano makali yalianza tena mwezi uliopita karibu na mji wa Goma, Mji mkuu wa Kivu Kaskazini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live