Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MCA anayeishi na HIV ambaye anatumia maisha yake kuwapa tumaini waathriwa

C1594ee6f91ede27 MCA anayeishi na HIV ambaye anatumia maisha yake kuwapa tumaini waathriwa

Thu, 27 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mary Goretti ni Mwakilishi wa Wadi katika Kaunti ya Uasin Gishu ambaye anaishi na virusi vya Ukimwi

- Mama huyo wa watoto sita ambaye aligundua hali yake mwaka 1999, alijitolea mhanga kutoa msaada na kuwatia moyo wagonjwa wenzake wa virusi vya Ukimwi

- Alishiriki katika mbio za baiskeli na kutuzwa kwa kumaliza wa kwanza

Wakati virusi vya ugonjwa wa Ukimwi viliripotiwa nchini Kenya, picha za vyombo vya habari viliwaonyesha waathiriwa wa ugonjwa huo kama watu waliobaki mifupa na wasiokuwa na afya.

Miongoni mwa wagonjwa nchini Kenya ambao walitibiwa na shirika lisilo la kiserikali la Ampath na kufaulu, ni Mary Goretti Boroswa.

Goretti, ambaye ni diwani mteule katika Kaunti ya Uasin Gishu alianza matibabu mwaka 2002.

Baada ya kukubali hali yake, afya yake ilikuwa bora na kushiriki kwenye mashindano ya baiskeli ili kutangaza hali yake ya HIV.

Licha ya unyanyapaa kuhusiana na hali yake, mwalimu huyo aliamua kujitolea kuwa balozi wa Ukimwi.

"Imekuwa safari ngumu lakini kuishi na virusi imenisaidia kuwafikia walioathirika na virusi hivyo kuwahimiza kukubal hali yao na kuishi maisha bora yenye afya kwa kila mtu," alisema.

Mama huyo wa watoto sita alisema aligundua hali yake mwaka 1999, wakati alijifungua watoto pacha.

Hata hivyo, alifichua kwamba alishuku alikuwa na virusi vya Ukimwi lakini wakati huo hakutaka kujua hali yake.

"Niliwaita Mercy na Faith. Mercy kwa sababu Mungu alikuwa na huruma kwangu na Faith kwa sababu imani yangu kwa Mungu ilikuwa imara kuishi maisha ya kawaida," alisema Goretti.

Aliongezea kuwa habari hizo zilikuwa za kushtua kutokana na taarifa kwenye vyombo vya habari na namna umma inachukulia virusi hivyo.

Goretti alisema kuwa wakati aliamua kwenda kupimwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi (MTRH), aliagizwa kuingia katika Chumba nambari 179, ambapo aling'amua ukweli.

Alimpongeza Profesa wa AMPATH, Joe Mamlin ambaye alimtia moyo katika maisha yake mapya akiishi na HIV.

Mamlin mdiye alitambua bidii yake na kumunulia basikeli za kisasa za mashindano ambayo ilimsaidia kuwabwaga washindani wengine na kupata pesa.

Alisema ameshuhudia vifo kutokana na virusi vya Ukimwi vikipingua maradufu.

"Kwa sasa mimi ni mbunge katika serikali ya kaunti ya Uasin Gishu. Ninawakilisha kundi la watu wachache na pia nasimamia masuala ya HIV na kukabiliana na unyanyapaa unaouzingira," alisema.

Gorreti alijitolea mhanga kutoa msaada na kuwatia moyo wagonjwa wenzake wa virusi vya Ukimwi na pia anasomea shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Moi baada ya kumaliza shahada ya kwanza mwaka 2012.

Akiwa nguzo muhimu katika kuhamasisha jamii kuhusu HIV, ameibuka mama shupavu katika jamii.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke