Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MC Yamkuta Ukumbini Alipogundua EX Wake Ndo Bibi Harusi

Harusi?fit=925%2C686&ssl=1 MC Yamkuta Ukumbini Alipogundua EX Wake Ndo Bibi Harusi

Sat, 22 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

KISANGA kimezuka katika harusi eneo la Mwatate, Taita Taveta nchini Kenya baada ya jamaa aliyekuwa akisherehesha sherehe ya harusi hiyo kushindwa kuzungumza na kulazimika kuweka chini kinasa sauti (microphone) alipogundua kuwa ex wake ndiye aliyekuwa akiolewa.

Taarifa zinasema kuwa kisura alimtoroka jamaa kwa dharau akimwambia kwamba hawezi kuolewa na mtu maskini. Wageni wakiwa wamekusanyika katika harusi, MC huyo ambaye ni mwalimu na wengi wanamjua sana kutokaa na sauti nzuri na maneno ya kumtoa nyoka pangoni ila siku hizo alibaki amekauka mdomo.

Inasemekana kuwa mrembo aliyekuwa akiolewa alikuwa mpenzi wa zamani wa ticha huyo, lakini licha ya jamaa kujibidiisha kupiga vibarua na kumfurahisha demu wake, bado aliachwa mataani.

Stori zaidi zinaesema kwamba jamaa alipogundua anaongoza harusi ya mpenzi wake wa zamani aliyempenda kwa dhati aliingiwa na huzuni nyingi akashindwa la kusema.

Penyenye zinaarifu kwamba wawili hao hawakukosana walipoachana ila mrembo alijiondoa kwa upole na kuanza uhusiano na jamaa mwingine aliyekuwa na mkwanja mrefu.

“Heri niolewe na rubani. Mwalimu kama wewe unayekisifia Kiswahili chako na sauti nzuri utanipa nini?” Jamaa alikumbuka mrembo akimuuliza na hapo akaishiwa nguvu mwilini na kuangusha kipaza sauti.

Aliinama akakiokota lakini akaanza kukohoa, hata maji aliyoletewa hayakumfaa kitu. Hatimaye lofa aliamua kuweka pembeni microphone akiashiria kwamba hangeendelea na sherehe, huku bi harusi akionekana akimtazama na kutabasamu akifurahia mateso ya jamaa.

“Alinikataa aolewe na jamaa yule mwenye sura ya nyani! Jamani! Kumbe pesa ni sabuni ya roho!” Tich alisikika akisema huku akisaidiwa kuondoka jukwaani kwani alikuwa ameisha nguvu kabisa.

Waliomsikia walimuonea huruma ila hakuna jinsi wangeweza kumsaidia. “Mbona mademu wanatesa majamaa hivi jamani?”

Jamaa mmoja alisema kwa huruma. “Lakini pia ukiachwa achika tu na ukubali,” demu mmoja naye alimjibu. Semasema zinaarifu kwamba jamaa alipoata mpenyo, alitumia mlango wa nyuma kutoweka katika sherehe hiyo.

Chanzo: globalpublishers.co.tz