Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

M23 yashtumu jeshi la DRC kwa kushambulia maeneo ya raia kwa mabomu

M23 Yashtumu Jeshi La DRC Kwa Kushambulia Maeneo Ya Raia Kwa Mabomu M23 yashtumu jeshi la DRC kwa kushambulia maeneo ya raia kwa mabomu

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Kundi la waasi la M23 limeshutumu wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kushambulia kwa mabomu maeneo ya raia Mashariki mwa nchi hiyo.

Katika taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari, kundi la waasi linadai kuwa DRC "na mamluki wanatumia helikopta za mashambulizi, ndege za kivita, vifaru vya kivita, na mizinga mikubwa ya risasi kulipua maeneo yenye wakazi wengi chini ya udhibiti wa M23."

Kundi hilo la waasi - ambalo jopo la kimataifa la wataalamu wa Umoja wa Mataifa linasema linafadhiliwa na Rwanda - linashikilia maeneo kadhaa mashariki mwa nchi hiyo, na limekuwa likihusika katika mapigano makali na jeshi la nchi hiyo katika wiki za hivi karibuni.

Mamia ya maelfu ya raia wamefurushwa kutoka maeneo haya katika mwaka uliopita kwa sababu ya mapigano hayo.

Chanzo: Bbc