Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

M23 wateka mji wa mpakani na Uganda

M23 Wateka Mji Wa Mpakani Na Uganda.png M23 wateka mji wa mpakani na Uganda

Mon, 5 Aug 2024 Chanzo: Voa

Waasi wa M23 wameuteka mji mmoja wa mpakani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bila mapigano Jumapili, duru za ndani zimesema, siku ambayo usitishaji mapigano kati ya DRC na nchi jirani ya Rwanda ulikusudiwa kuanza kutekelezwa.

Mji wa Ishasha uliopo mpakani na Uganda, umekuwa wa karibuni zaidi kuangukia mikononi mwa kundi hilo linaloungwa mkono na Rwanda.

M23 imeteka maeneo mengi katika jimbo la Kivu Kaskazini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo toka ilipoanzisha mashambulizi yake mwishoni mwa 2021.

Ishasha imechukuliwa bila upinzani na kuwa chini ya udhibiti wa M23, kiongozi wa mashirika ya kiraia Romy Sawasawa ameiambia AFP.

Maafisa wa polisi wa Congo walivuka mpaka hadi Uganda wakikimbia waasi waliokuwa wengi na silaha za kutosha.

Chanzo: Voa