Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

M23 :Mpatano ya Rwanda, DRC hayatusumbui

Mtoto Wa Museveni Anaunga Mkono M23 M23 :Mpatano ya Rwanda, DRC hayatusumbui

Fri, 25 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la waasi wa M23 limesema kuwa halihusiki na tangazo la usitishwaji mapigano lililotolewa mjini Luanda kwa madai kuwa hakukuwa na mwakilishi wao kwenye mkutano wa kilele wa Luanda.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Vincent Biruta walihudhuria mkutano mdogo wa kilele mjini Luanda Jumatano ambao uliwataka waasi kusitisha mapigano kufikia Ijumaa jioni ikiwa ni pamoja na kujiondoa kwenye maeneo yote yanayokaliwa na M23 na kurejea kwenye maeneo yao ya awali.

Msemaji wa kisiasa wa M23, Lawrence Kanyuka amesema waliona taarifa hiyo kwenye mitandao ya kijamii hivyo maazimio hayo hayawahusu huku wakitoa wito wa mazungumzo ya moja kwa moja na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live