Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lungu atamani Urais tena Zambia

Edgar Lungu Lungu atamani Urais tena Zambia

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu amesema anarejea katika siasa miaka kadhaa tangu astaafu kama Rais wa Zambia na kiongozi wa Chama cha Patriotic Front.

Tayari serikali ya Zambia imeondoa marupurupu ya kustaafu ya Rais huyo wa zamani kufuatia uamuzi wake wa kurejea katika siasa kali.

Bw Lungu alipoteza urais kwa Hakainde Hichilema mwaka 2021, na kisha akatangaza kustaafu.

Baada ya miaka sita madarakani aliondoka nchini akikabiliwa na masuala mazito ya kiuchumi akiwa na taifa lenye deni kubwa zaidi barani Afrika.

Kurejea kwake katika siasa kunaweka mazingira mazuri ya kinyang'anyiro cha urais 2026.

Tangu wakati huo Lungu amezindua azma ya kukiongoza chama cha Patriotic Front, chama kilichoshika madaraka kuanzia 2011 hadi Lungu aliposhindwa na Hichilema.

Kwa sasa chama hicho kina mzozo wa uongozi. Wafuasi wa Lungu wanamtuhumu aliyekuwa meya wa Lusaka Miles Sampa kwa kunyakua urais wa chama kwa amri ya Hichilema.

Lungu pia anaishutumu serikali kwa kukiuka haki zake. Amezuiwa na polisi kuodoka nchini hata kwa sababu za kimatibabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live