Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lungu: Hichilema ameshindwa kuongoza

Hichilemaaa Lunguu.png Lungu: Hichilema ameshindwa kuongoza

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu ametoa wito kwa raia kwenye taifa hilo kuitisha uchaguzi wa mapema, akimtuhumu mrithi wake Hakainde Hichilema, kwa kushindwa kuongoza nchi.

Aidha Lungu pia anamtuhumu rais Hichilema kwa kushindwa kukabiliana na msambao wa maambukizo ya kipindupindu, ambao umesababisha vifo vya karibia watu 600 tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

Wakati akizungumza na wanahabari, Lungu amewataka wapiga kura kushinikiza kufanyika kwa uchaguzi huo wa urais mapema.

Kwa upande wake msemaji wa serikali Cornelius Mweetwa ametupilia mbali matamshi ya rais huyo wa zamani akitoa wito wa raia wa Zambia kumpa muda rais wa sasa ilikutekeleza agenda zake alizotoa wakati wa kampeni.

Aidha serikali imemtuhumu kiongozi huyo wa zamani kwa kuharibu uchumi wa nchi yake wakati wa kipindi chake cha miaka sita afisini.

Mwezi Oktoba mwaka uliopita, Lungu alitangaza kurejea tena katika ulingo wa kisiasa, hatua ambayo ilipelekea serikali kuwaondoa mafao yake.

Lungu alikuwa amestaafu kutoka kwa siasa mwaka wa 2021 baada ya kushindwa kutetea kiti chake katika uchaguzi mkuu wa urais.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live