Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukaku aweka mambo hadharani

89986 Lukaku+pic Lukaku aweka mambo hadharani

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MILAN, ITALIA. STRAIKA, Romelu Lukaku amefichua kwamba mtu wa kwanza kwenye kikosi cha Manchester United kumwambia kwamba amechoka na aachana na timu hiyo ni kiungo Mfaransa, Paul Pogba. Straika huyo Mbelgiji alisema kwamba alichoshwa na vitendo vya kukosolewa tu yeye kwa muda wake wote aliokuwa Old Trafford. Kutokana na hilo, Lukaku aliamua kuondoka zake kwenda kujiunga na Inter Milan kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi kwa ada ya Pauni 73 milioni na tangu wakati huo amefunga mabao 12 katika mechi 17 alizocheza kwenye Serie A na kuisaidia timu kuongoza ligi. Man United huko kwa upande wao wanawaza kumsajili mshambuliaji mwingine wa kuja kuziba pengo lake katika dirisha la Januari na wamekuwa wakihusishwa na mpango wa kumnasa staa wa Red Bull Salzburg, Erling Haaland . Lukaku alifunga mabao 42 katika mechi 96 za michuano yote alizoitumikia Man United kwa misimu miwili, lakini anadhani mashabiki waliokuwa wakitazama zaidi nafasi alizokuwa akikosa kuliko alizofunga. Alichofanya alimwambia swahiba wake, Pogba kwamba anaondoka wakati walipokuwa wakielekea kwenye maandalizi ya msimu mpya huko Australia. "Nilimwambia, nimechoka," alisema Lukaku. "Nilifunga bao dhidi ya Real Madrid kwenye European Super Cup, lakini nikakosa nafasi kadhaa pia. Ilikuwa nongwa, kila kitu amekosa ile nafasi. Nilifunga dhidi ya West Ham kwenye mechi yangu ya kwanza ya Ligi Kuu England, lakini baada ya hapo kilichofuata, sikuwa nafahamu mambo yanakwendaje." Lukaku amekubaliana na Cristiano Ronaldo akidai kwamba kufunga bao kwenye Serie A ni ngumu kuliko kwenye Ligi Kuu England.

Chanzo: mwananchi.co.tz