Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lugha ya Kiingereza ni kikwazo kwa wakimbizi Uganda

Lugha Ya Kiingereza Ni Kikwazo Kwa Wakimbizi Uganda Lugha ya Kiingereza ni kikwazo kwa wakimbizi Uganda

Thu, 20 Jun 2024 Chanzo: Voa

Moja ya vikwazo vikuu kwa wakimbizi wa Sudan kujaribu kujenga maisha mapya nchini Uganda ni lugha. Baadhi ya takriban watu 40,000 ambao wamewasili katika miezi ya karibuni walikuwa na wanajua kiingereza kidogo lakini hakiwasaidii kupata ajira au kuingia kwa urahisi katika jamii za Uganda. Kundi la kuwawezesha wanawake lililoko katikati mwa Uganda linajaribu kubadili hilo.

Somo la msingi la Kiingereza, linafundishwa kwa wafanyakazi wa zamani serikali na watoto wao.

Wakimbizi hawa wanaozungumzza lugha ya Kiarabu kutoka Sudan ambao wana hamu kubwa ya kujifunza Kiingereza ili kurahisisha kipindi chao cha mpito nchini Uganda.

Miongoni mwa ni Razan Abdulrahim Muhammad, mhandisi wa kemikali na mama wa watoto wanne. Amekimbia nchini Sudan mwezi Machi, na alipoteza mawasiliano na mume wake.

Aliambia Sauti ya Amerika kuwa “Nataka kujiweka vizuri, kuwa na uwezo wa kuomba kazi yoyote ili niweze kuwahudumia watoto wangu.”

Katika kila darasa la wanafunzi 50 wanahitaji walau miezi mitatu kujifunza lugha. Asmahan Ahmed lazima achanganye Kiarabu na Kiingereza kwa wanafunzi wake kuelewa kwa urahisi.

Kukiwa na vifaa vichache, mhandisi wa zamani wa majengo anafundisha somo la Kiingereza kwa kutumia sauti.

Wakimbizi wengi, anasema, wanajifunza Kiingereza kwa kiwango kidogo shuleni wanapowasili nchini Uganda.

Asmahan Ahmed, ni Mwalimu na mkimbizi kutoka Sudan alisema “Ilikuwa ngumu kwetu sisi kuwasiliana na kukitumia kwa malengo ya kijamii. Tumeona ugumu kujieleza wenyewe, tunachofahamu, tunachotaka, tunachohitaji.” Naye Dawla Hussein Hassan ambaye alikoseshwa makazi kwa mara ya kwanza kutoka Sudan mwaka 2011 wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Aliomba hifadhi nchini Sudan Kusini, lakini mzozo katika nchi hiyo ulimsukumu na kuingia nchini Uganda mwaka 2014.

Hivi sasa ni mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Kandaakiat, ili kuwawezesha wanawake, amekuwa akifaya kazi kuboresha maisha ya wakimbizi wapya wa Sudan wanaowasili.

Hassan anaelezea kwamba mapambano na lugha ya Kiingereza yamewaacha wakimbizi wengi wakiwa wamefadhaishwa, bila ya kujali elimu yao na ujuzi wao.

“Wanahitaji msaada wa kweli kujiweka vizuri katika jamii hii, na kuuhisi utu wao. Kwasababu mimi kama daktari, siwaelezi madaktari wenzagu ninavyohisi, kama mgonjwa. Kwasababu lugha ni kikwazo, na hapo inakuja aibu. Na mengi ni kwamba utahisi kama unanyanyasika.” Alisema mkurugenzi huyo mtendaji wa Taasisi ya Kandaakiat.

Kuanzia mwanzoni mwa Juni, Uganda imeandikisha zaidi ya wakimbizi 39,000 kutoka Sudan, huku asilimia 70 wakiwa ni wanawake na watoto.

Paul Zbigniew Dime, afisa mwandamizi wa hiadhi katika shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa nchini Uganda, anafanyakazi na serikali ya Uganda ili kusaidia madaktari na maprofesa wakimbizi wanapewa leseni na kuidhinishwa.

“Tumefanikiwa kuwapata wasifu wa wafanyakazi hadi sasa, katika makazi ya Kiryandogo, mjini Kampala. Tunafanya majadiliano, na tunafanyakazi na wizara ya afya, wizara ya elimu na michezo ili waweze kufanya shughuli zao hapa nchini Uganda.” Alisema Dime.

Hassan ana matumaini kwamba kwa msaada zaidi na upanuzi wa kituo cha mafunzo, wakimbizi wengi watakuwa na uwelewa mzuri wa lugha ya Kiingereza ili kujitayarisha kwa kile ambacho hivi sasa kinaoenkana kama mustakbali usiokuwa na uhakika, alisema mkurugenzi huyo mtendaji wa Taasisi ya Kandaakiat.

Chanzo: Voa