Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Louisa Hanoune ajiondoa kinyang'anyiro cha urais Algeria

Louisa Hanoune Louisa Hanoune

Mon, 15 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Louisa Hanoune, Kiongozi wa Chama cha wafanyakazi wa Algeria (Trotskyist), ambaye alifungwa Gerezani kutokana na vuguvugu la Maandamano ya Hirak mwaka 2019, alitangaza Jumamosi Julai 13 kujiondoa katika mbio za Urais katika Uchaguzi ujao.

Louisa Hanoune, Mgombea Urais mwaka wa 2004, 2009 na 2014, hakutoa maelezo zaidi, lakini alionyesha kuwa uamuzi wake ulitokana na taarifa alizo nazo.

Rais aliyepo madarakani, Abdelmadjid Tebboune(78), alitangaza kwamba atawania Urais tena kwa kuzingatia matamanio ya vyama vingi, mashirika ya kisiasa na yasiyo ya kisiasa, na vijana.

Abdelmadjid Tebboune, ndiye anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi ujao baada ya kushinda uchaguzi uliopita kwa 58% ya kura.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live