Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lori laua madereva bodaboda zaidi ya 10

Screen Shot 2023 04 08 At 10.png Lori laua madereva bodaboda zaidi ya 10

Sat, 8 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu kadhaa wamepoteza maisha baada ya lori lililokuwa likisafirisha changarawe kupoteza mweleke0 na kugonga kundi la bodaboda waliokuwa wameegesha eneo lao (kijiweni) mjini Migori nchini Kenya.

Tukio hilo la asubuhi ya Jumamosi - Aprili 8,2023 limeshuhudia umati mkubwa wa watu ukimiminika eneo la tukio ili kuwanusuru majeruhi na kuwakimbiza hospitalini kwa matibabu.

Kwa mujibu wa raia mmoja aliyeshuhudia na kuzungumza na runinga ya TV47, breki za lori hilo zilifeli na kuingia katika kundi hilo la bodaboda ambao walikuwa wanasubiri abiria.

Ajali hiyo imefanyika karibu na shule ya msingi ya Migori. Eneo la tukio lilikuwa limejaa damu na miili. Vyuma pia vilikuwa vimetapakaa eneo hilo.

Eneo la tukio linaripotiwa kuwa na zaidi ya miili kumi huku ambulansi na wazima moto kutoka kwa serikali ya kaunti ya Migori wakifika eneo la ajali hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live