Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lori la mikate na juisi yagongana, wananchi wagombania

MKATE JUICES Lori la mikate na juisi yagongana, wananchi wagombania

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kumeibuka hali ya taharuki katika mji wa Juja huku wakazi wakihaha kuokota juisi na mkate baada ya lori mbili zilizokuwa zimebeba vyakula kugongana kwenye barabara kuu ya Thika Superhighway.

Ajali hiyo iliyotokea jana Machi 25, 2025 ilisababisha bidhaa nyingi kumwagika barabarani, na kuvutia umati wa watazamaji na watu wanaopenda kunyakua vitu vya bure.

Umati wa watu ulikusanyika eneo la tukio Video iliyoshirikiwa kwenye Juja People na Wamigwi Agnes ilinasa wakazi wakipora vyakula.

Malori hayo mawili, moja likiwa limesheheni juisi mbalimbali na lingine mkate, yaligongana na kupinduka na kusababisha tukio hilo.

Ndani ya dakika chache, umati mkubwa ulikuwa umekusanyika mahali hapo, wakichukua mikate mingi kadiri wangeweza kubeba.

Licha ya juhudi za polisi kudhibiti hali hiyo, umati wa watu ulipanda hata kwenye lori ili kupata bidhaa zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live