Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lofa akimbilia huduma za mganga kumrejesha kipusa pendoni

Ddfd5fb917680598 Lofa akimbilia huduma za mganga kumrejesha kipusa pendoni

Fri, 9 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Jamaa mmoja kutoka Makima, Embu aliona moto baada ya kushambuliwa kwa kichapo na kipusa aliyekuwa mpenzi wake kwa kumwendea kwa mganga.

Inasemekana jamaa aliingia na wivu kidosho huyo alipoanza kutongozwa na lofa mwingine na hivyo akaamua kwenda kwa mganga kutafuta ndumba ili amrejeshe pendoni.

Kwa mujibu wa Taifa Leo, jamaa aliamua kufanya hivyo kwani kisura alikuwa na mimba ambayo alishuku ni yake.

Penyenye zinaarifu kuwa kipusa aligundua jamaa alikuwa amemwendea kwa mganga na akaamua kukabiliana naye.

Alifululiza moua kwa moja hadi nyumbani kwa akina jamaa na kumkuta akiwa na familia yake.

Mwanzo jamaa alipomuona alijawa na furaha akidhani hatimaye amefanikiwa kumfanya demu amrudie tena.

“Karibu nyumbani. Nimeishi kwa muda mrefu bila kukuona tangu tulipoachana,” lofa alimwambia demu huku akitabasamu.

Hata hivyo aishtuka sana kisura alipoanza kumfokea vikali.

“Sitaki kukaribishwa. Sijakuja hapa kucheka na wewe, nimekuja kukufunza adabu. Ulienda kwa mganga kufanya nini? Ulidhani mganga atakusaidia nikurudi? Utaacha ushenzi wako leo,” kidosho alichemka huku akimwnagushia lofa kichapo mbele ya dada na wazazi wake.

Semasema zinaarifu kuwa jamaa alipatwa na aibu kubwa akatamani ardhi ipasuke immeze mzima mzima lakini dua zake ziliambulia patupu.

“Nisamehe sitarudia tena. Jamani! Ni mambo ya shetani sio kutaka kwangu,” jamaa alilia.

“Mimi nitakutwanga hadi huyo shetani akuondokee. Siku nyingine usiwahi kuniendea kwa mganga. Ulidhani sitajua kwani? Tuliachana kwa sababu ya tabia kama hii ya kupenda nguvu za giza,” kisura aliwaka.

Papo hapo alimwelezea jamaa kwamba mimba aliyokuwa amebeba hakikuwa yake.

“Wewe ni bwege huwezi hata kufunga bao hata goli likiachwa wazi,” mrembo alimkjeli jamaa.

Iliwabidi wazazi kuomba msamahakwa niaba ya mwanao ambaye walilazimika kumfungua ndani ya nyumba mijeledi ilipozidi.

Kisura alimkomesha jamaa na kisha akashika njia na kwenda zake alikotoka.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke