Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ligi Kuu Rwanda kuendelea

09d75858207be4577fa761d468ccbe08 Ligi Kuu Rwanda kuendelea

Wed, 17 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KATIBU MKuu wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA), François-Régis Uwayezu anasema kuwa maandalizi yanaendelea kwa ajili ya kuendelea tena na Ligi Kuu ya Rwanda iliyosimama tangu Desemba mwaka jana.

Uwayeza anasema kuwa ligi hiyo sasa inaweza kuendelea mwezi ujao baada ya kusimama kwa miezi kadhaa .

Wizara ya Michezo ilisimamisha ligi kubwa zote tangu Desemba 12, 2020 baada ya klabu kushindwa kufuata miongozo iliyotolewa na serikali kwa ajili ya kujikinga na Covid-19.

Imebanishwa kuwa wadau zikiwemo klabu, Wizara ya Michezo na Ferwafa, na taasisi zingine zinazohusika na soka zilikutana kujadili lini ligi hiyo itaendelea.

Uwayezu alisema uamuzi wa mwisho kuhusu kuendelea kwa ligi hiyo bado haujafikiwa, lakini kuna nafasi kubwa ligi itaendelea mwezi ujao.

“Kumekuwa na majadiliano mengi lini ligi inaweza kuendelea na itategemea kama klabu zitaweza kukamilisha au kufuata taratibu za kujikinga na Covid-19 huko mbeleni. Tuna matumaini kuwa ligi itaendelea mwezi ujao.

Akizungumza na waandishi wa habari Desemba 16, 2020, akinukuu hatua za kujikinga na Covid-19, waziri wa Michezo, Aurore Mimosa Munyangaju alisema ligi itaendelea.

“Ligi itaendelea haraka iwezekanavyo kwa sasa mazungumzo yanaendelea kati yetu na Shirikisho la Soka la Rwanda.”

Desemba 24, 2020, FERWAFA iliandaa mkutano wa ushauri na timu za daraja la kwanza, zote zilikubaliana kuwa zinaweza kuendelea na ligi, zikiahidi kutorudia makosa yaliyopita yaliyosababishwa kusimamishwa kwake.

Mapema mwaka huu, Rais wa FERWAFA Jean-Damascène Sekamana alisema kuwa walipanga ligi kuendelea Februari baada ya kuitaarifu Wizara ya Michezo kuwa hatua zao zitatekelezwa.

Raundi ya kwanza ya mechi za ligi ilifutwa baada ya siku tatu, huku mechi nane zikiahirishwa, zikiwemo nne kwa sababu ya Covid-19.

Chanzo: habarileo.co.tz