Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Licha ya madeni makubwa, Kenya yaongoza kwa idadi ya matajiri Afrika Mashariki

Wealth Report 2021 Social Sharing Licha ya madeni makubwa, Kenya yaongoza kwa idadi ya matajiri Afrika Mashariki

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kenya imezidia kuongeza idadi ya wananchi mamilionea licha ya nchi hiyo kuwa na madeni makubwa kupita nchi zote za Afrika Mashariki. Kwa mujibu wa takwimu za Global Wealth kutoka Benki ya uwekezaji nchini Uswizi, inaonesha kila mwananchi wa Kenya anadaiwa Tsh. 1,212,575.50 kwenye deni la taifa.

Kenya imetajwa kwenye nchi zenye taarifa mbaya za kifedha ikiwemo matumizi mabaya ya mikopo ambayo yanatajwa kama moja ya sababu za nchi hiyo kuwa na idadi kubwa ya mamilionea huku walipa kodi wakibebeshwa mzigo mkubwa wa 30% kwenye bajeti ya taifa ambayo hugharimu zaidi ya Tsh. Bilioni 41 kwa siku.

Mwaka 2020 idadi ya Wakenya wenye utajiri wa Tsh. Bilioni 69 ukijumuisha nyumba zao walikua 90, idadi ikiwa imeshuka kutoka 106 mwaka 2019 na sababu ikitajwa kuwa ni kutokana na athari za COVID-19 kwa mujibu wa taarifa za Knight Frank Wealth.

Nchi ya Kenya inashika nafasi ya nne barani Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya matajiri ikiongozwa na Nigeria, South Africa na Egypt.

Utafiti uliofanywa na Swiss investment Bank Institute, uliotoka hivi karibuni umeonesha kuwa pamoja na kuelemewa na madeni ya mikopo yanayotajwa kufikia Dola za Marekani Bilioni 64.22 (zaidi ya Tsh. Trilioni 140), nchi hiyo ndiyo utajiri mkubwa kwenye nchi za Afrika Mashariki. Ikikadiriwa kuwa na utajiri wa dola za Marekani Bilioni 338 hadi kufikia mwaka 2020.

Hii inamaanisha kuwa watu wa zima nchini Kenya wanamiliki kuanzia Dola za Marekani 12,313 na wastani wa chini ni Dola 3,683.

Kenya inafuatiwa na Rwanda ambapo kiwango cha utajiri cha mtu mzima ni dola 4,188; Tanzania Dola 3,647, Uganda Dola 1,994; Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Dola 1,240 na Burundi Dola 728.

Utafiti huo pia umeonesha kuwa kila mtu mzima nchin Tanzania anadaiwa dola 137, ikifuatiwa na Rwanda ($135), Uganda ($107), Burundi ($37) na Congo DR ($36). Kwa mujibu waripoti hiyo pia, DR Congo inakadiriwa kuwa na idadi ya watu wazima Milioni 39.74, Tanzania Milioni 27.74, Kenya Milioni 27.47, Uganda watu wazima Milioni 19.83, Rwanda Milioni 6.58, na Burundi watu wazima Milioni 5.38.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live