Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Licha ya kashfa ya "Pandora Papers" Rais Uhuru apewa tuzo ya uongozi bora

8bc1d3460830146c Licha ya kashfa ya "Pandora Papers" Rais Uhuru apewa tuzo ya uongozi bora

Thu, 7 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Ikiwa n siku chache tangu Rais Kenyatta atajwe kwenye orodha ya Pandora Papers inayohusisha viongozi na watu maarufu wanaoficha pesa nje ya nchi, serikali ya Barbados imempa tuzo Rais Uhuru Kenyata kwa uongozi bora katika kukuza biashara ya ulimwenguni.

Tuzo ya 'Order of Freedom of Barbados' iliyokabidhiwa Rais Uhuru Kenyatta ndio kubwa zadi kutoka kwa wananchi wa Barbados na mataifa ya kigeni kwa huduma za mfano bora.

Rais Kenyatta amesema ataendelea kuhimarisha uhusiano kati ya Afrika na CARICOM na kuhakikisha kuwa Wafrika wanafanya kazi pamoja.

Kenyatta alienda Barbados baada ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa rasmi kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Siku ya Jumatano, Oktoba 6,

Tuzo hiyo ilitolewa kwa Uhuru na gavana wa taifa hilo Dame Sandra Mason katika Jumba la Serikali mjini Bridgetown.

“Tuzo ya heshima ya Agizo la Uhuru wa Barbados inapewa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa mafanikio yake bora kama kiongozi wa ulimwengu, kujitolea kwake kuhimarisha biashara ya ulimwengu na maendeleo endelevu na juhudi za kuimarisha vifungo vya ushirikiano na urafiki kati ya Kenya na Jumuiya ya Karibiani, haswa uhusiano wa pande mbili kati ya Kenya na Barbados," ilisoma kinukuu hicho.

Rais alisema ataendelea kuhimarisha uhusiano kati ya Afrika na CARICOM na kuhakikisha kuwa Wafrika wanafanya kazi pamoja.

"Azimio na lengo letu ni kuona watu wote wenye asili ya Kiafrika wakikusanyika pamoja, kuweza kusimama pamoja na kuweza kupigania haki zetu, uhuru na nafasi yetu katika maswala ya ulimwengu," alisema kiongozi wa taifa.

Waliohudhuria ni Waziri Mkuu wa Barbados, Mia Mottley, mawaziri Raychelle Omamo (Wizara ya Masuala ya Kigeni) na Monica Juma (Kawi).

Rais alisafiri Barbados baada ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa rasmi kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.

Rais na kikosi chake walitua katika mji mkuu wa Addis Ababa, Jumatatu, Oktoba 4, mchana wakiwa wameabiri Ndege ya Shirika la Kenya Airways.

Mnamo mwaka 2018, Uhuru alipokea tuzo spesheli kutoka kwa jamii ya Sikh kwa mchango wake katika kuleta umoja na amani nchini.

Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa tuzo za Sikh Awards 2018, na kukabidhiwa Uhuru na Navdeep Singh katika Ikulu ya Nairobi.

Akipokea tuzo hiyo, Uhuru alisema Kenya itaendelea kushirikina na jamii tofauti kwa maendeleo ya taifa na amani kote duniani.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke