Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Libya yawarejesha makwao wahamiaji haramu 248

Wahamiaji Watoto Wanachukuliwa Kama Watu Wazima Uhispania Libya yawarejesha makwao wahamiaji haramu 248

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idara ya Kudhibiti Uhamiaji Haramu ya Libya jana Jumanne iliwarejesha makwao wahamiaji haramu 248. Hayo ni kwa mujibu wa Mkuu wa Ofisi ya Uhamiaji ya idara hiyo, Badraddin Ben-Hamed.

Ben-Hamed ameongeza kuwa, miongoni mwa wahamiaji hao, wamo 20 waliorejeshwa kwao Niger kwa ndege, huku 128 waliobakia wakirejeshwa kwao Chad kwa njia ya nchi kavu.

Naye Naibu Rais wa Baraza la Uongozi la Libya, Musa al-Kuni, ambaye ameitembelea na kukagua kazi za idara hiyo wakati zoezi la kuwarejesha makwao wakimbizi hao lilipokuwa linatekelezwa amepongeza jambo hilo na kusisitiza kuwa, zoezi hilo linafanyika kwa malengo ya kibinadamu.

Amesema: "Ninatoa shukrani zangu kwa wale wote wanaofanya kazi katika Idara ya Kudhibiti Uhamiaji Haramu kwa juhudi zao za kuwaandalia wahamiaji hao mazingira mazuri na ya kibinadamu ya kimaisha, licha ya changamoto nyingi nzito wanazokabiliana nazo ikiwa ni pamoja na uwezo mdogo na suhula chache. Wakimbizi wa Bangladesh wakirejeshwa kwao kutokea Libya

Wahamiaji wengi, hasa wa nchi za Afrika za kusini mwa Jangwa la Sahara wanaitumia Libya kama moja ya njia kuu za kuvuka Bahari ya Mediterania kuelekea kwenye fukwe za Ulaya, kutokana na ukosefu wa usalama na machafuko yaliyoikumba Libya tangu wakati wa kampeni za kuangushwa utawala wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Ripoti za Shirika la Kimataifa la Uhahmiaji zinasema kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi hivi sasa, wahamiaji haramu 15,057 wameokolewa baharini na kurudishwa nchini Libya.

Pupa ya kutaka kupata maisha mazuri barani Ulaya yanapelekea baadhi ya watu wenye mitazamo finyu na tamaa ya kupindukia kuhatarisha maisha yao na kujiingiza kwenye hatari nyingi. Wengi wao huishia kupoteza maisha baharini au kwenye mikono ya magenge hatari ya magendo ya binadamu na kupigwa mnada masokoni kama bidhaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live