Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Libya yawahukumu kifo wanachama 17 wa ISIS

Hukumu Pc Data Libya yawahukumu kifo wanachama 17 wa ISIS

Tue, 20 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama moja nchini Libya imewahukumu kifo wanachama 17 wa kundi la kigaidi la ISIS (Daesh).

Aidha mahakama hiyo ya mjini Tripoli jana Jumatatu iliwahukumu wanachama wengine 14 wa ISIS kifungo cha maisha jela, huku wengine kadhaa wakisukumwa jela kwa miaka kadhaa.

Sehemu ya hukumu iliyosomwa dhidi ya watu hao waliohukumiwa jana inasema: Mumepatikana na hatia ya kufanya vitendo vinavyohusishwa na IS, kwa kuhujumu dola na amani ya kijamii, na pia kufanya jinai kwa silaha katika mji wa magharibi wa Sabratha na viunga vyake.

Korti hiyo ya Libya ambayo haijataja uraia wa wanachama hao wa ISIS imesema, waliopatikana na hatia waliuawa watu 53, mbali na kuharibu majengo ya umma na 'kuwapoteza' makumi ya watu.

Hujuma za wanamgambo wa ISIS nchini Libya Libya imekuwa uwanja wa machafuko tangu Jeshi la Nchi za Magharibi NATO kwa kuongozwa na Marekani, kuingilia kijeshi nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika na kumuondoa madarakani Kanali Muammar Gaddafi.

Tangu wakati huo, nchi hiyo imekosa usalama huku makundi ya kigaidi hususan Daesh (ISIS) yakitumia machafuko hayo kujipenyeza ndani ya taifa hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live