Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Libya yaiangukia UN Uchaguzi Mkuu

Kuraaa.png Libya yaiangukia UN Uchaguzi Mkuu

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya ameutaka Umoja wa Mataifa uunge mkono juhudi za serikali yake za kutaka kuitishha uchaguzi na kuinasua nchi hiyo kutoka katika mkwamo wa kisiasa.

Abdul-Hamid Dbeibah amemtaka Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuisaidia Libya ili iweze kuitisha na kuendesha zoezi la uchaguzi ambalo kuakhirishwa kwake kumezidi kuitumbukiza nchi hiyo katika mkwamo wa uongozi.

Mkuu huyo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya amemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atume timu ya wataalamu ili kutathmini hali ya mambo na kuweko uratibu baina yake na serikali jambo ambalo amesema, litaandaa mazingira ya kufanyika kwa mafanikio uchhaguzi huo.

Dbeibah amesema, serikali yake ina hamu ya kuendesha uchaguzi wa Rais na Bunge ili wananchi wapate fursa ya kuchagua wawakilishi wao na hivyo kuhitimisha mzozo wa sasa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Filihali Libya ina serikali mbili ambapo kila serikali kati ya hizo inadai kwamba, ndio halali na inayopaswa kushika hatamu za nchi.

Abdul-Hamid al-Dbeibah, Mkuu wa Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya anashikilia hatamu za uongozi kwa zaidi ya mwaka mmoja kufuatia makubaliano ya kisiasa yaliyofikkiwa na ambayo yalisimamiwa na Umoja wa Mataifa

. Katika upande mwingine, Bunge la Libya katika eneo la Tobruk mwezi Machi mwaka jana lilimpigia kura ya kuwa na imani Fathi Bashagha kwa ajili ya kuchukua wadhifa wa Waziri Mkuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live