Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Libya: Wenye hasira kali wachoma bendera ya Israel

Israel Bendera Libya: Wenye hasira jali wachoma bendera ya Israel

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika kuonyesha upinzani dhidi ya serikali kuhusu kuhalalisha mkutano wake na utawala wa Israel, waandamanaji wenye hasira wa Libya wamechoma moto bendera ya Israel wakati wa maandamano katika miji ya Al-Zawiya na Tajoura.

Katika mji wa mashariki mwa Libya wa Tajoura, waandamanaji wamefunga barabara kuu kupinga mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala haramu wa Israel kuhusu kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya pande mbili. Wametishia kuzidisha hatua zao, ikiwa ni pamoja na kufunga njia ya reli kuelekea makao makuu ya serikali ya Waziri Mkuu Abdul Hamid al-Dbeibeh.

Habari za mkutano huo zimezua wimbi la hasira miongoni mwa Walibya kwenye mitandao ya kijamii, wakilaani kile wanachokiona kama kitendo cha "usaliti" kilichofanywa na kila mtu aliyehusika. Katika taarifa yake kuhusu tukio hilo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Libya imesisitiza kuhusu kufungamana na sera ya Al-Quds (Jerusalem) kuwa mji mkuu wa milele wa Palestina, na kuongeza kuwa huu ni msimamo thabiti ambao hauwezi kugeuzwa. Wizara ya Mambo ya Nje ya Libya imesema kwamba Waziri wa Mambo ya Nje Najla Al-Mangoush amekataa kufanya mikutano yoyote na taasisi yoyote inayowakilisha utawala wa Kizayuni wa Israe, na anabakia kuwa thabiti kuhusu msimamo huo.

Wizara hiyo imedai kuwa kilichotokea Roma ni mkutano wa kawaida usio rasmi na ambao haukupangwa wakati wa mkutano wa Al-Mangoush na Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia. Kwa upande wake, Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Abdul Hamid al-Dabaiba, amemsimamisha kazi Waziri wa Mambo ya Nje Al-Mangoush kama tahadhari huku uchunguzi ukiendelea. Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Israel na Libya, ulioelezewa na vyombo vya habari vya Israel kama "wa kihistoria," umeibua hasira kote Libya. Mkutano huo wa siri ni wa kwanza kufanyika moja kwa moja baina ya mawaziri wa mambo ya nje wa utawala haramu wa Israel na Libya. Wakati huohuo, muambata wa zamani wa vyombo vya habari katika ubalozi wa Libya nchini Tunisia, Jamal Al-Kafali, amenukuu chanzo ndani ya serikali ya Dbeibah kikisema: "Al-Mangoush alikuwa katika mkutano na mwenzake wa Italia wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel alipowasili." Amesema madai yaliyotolewa na vyombo vya habari vya Israel kuhusu nia ya Al-Mangoush kushirikiana kikamilifu na utawala haramu wa Israel ni ya uongo kabisa. Amesisitiza zaidi kwamba Waziri Mkuu wa Libya ameamuru uchunguzi wa haraka ufanyike kuhusu tukio hilo, na taarifa ya baadaye itolewe na Waziri wa Mambo ya Nje.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live