Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Libya: Waziri akimbia nchi baada ya kutumbuliwa!

Waziri Libya Akimbia Libya: Waziri akimbia nchi baada ya kutumbuliwa!

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya, Najla al Mangoush amekimbilia Uturuki baada ya Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya kumsimamisha kazi kwa kosa la kuonana na waziri wa mambo ya nje wa utawala wa Kizayuni nchini Italia.

Hayo ni kwa mujibu wa televisheni ya WION. ambayo imesema kwamba, al Mangoush amekiri kuwa amefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Israel kwa uratibu wa waziri wa mambo ya nje wa Italia, Antonio Tajani lakini amedai kuwa mazungumzo hayo hayakuwa rasmi na hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa.

Hata hivyo utawala wa Kizayuni unachukiza mno katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu kiasi kwamba, kitendo chochote cha kuwa karibu na Wazayuni kinapokewa kwa hasira kubwa.

Katika kuonyesha hasira zao dhidi ya serikali baada ya waziri wa mambo ya nje wa Libya kuonana na waziri huyo Mzayuni, wananchi wenye hasira wa Libya wamechoma moto bendera ya Israel na kulaani kitendo chochote cha kuwa karibu na utawala katili wa Israel Taarifa zinasema kuwa, Waziri Mambo Nje Libya, Najla al Mangoush amekimbilia Uturuki

Katika mji wa mashariki mwa Libya wa Tajoura, waandamanaji wamefunga barabara kuu kulalamikia kitendo cha Najla al Mangoush cha kukutana na Mzayuni huyo na kuapa kuendeleza maandamano yao ikiwa ni pamoja na kufunga njia ya reli kuelekea makao makuu ya serikali ya Waziri Mkuu Abdul Hamid al-Dbeibeh kama hatua kali dhidi ya Najla zisingechukuliwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Abdul Hamid al-Dabaiba, amemsimamisha kazi Waziri wa Mambo ya Nje Al-Mangoush kama tahadhari huku uchunguzi ukiendelea.

Wakati huohuo, mwambata wa zamani wa vyombo vya habari katika ubalozi wa Libya nchini Tunisia, Jamal Al-Kafali, amenukuu chanzo kimoja cha ndani ya serikali ya Dbeibah kikisema: "Al-Mangoush alikuwa katika mkutano na mwenzake wa Italia wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel alipowasili."

Amesema madai yaliyotolewa na vyombo vya habari vya Israel kuhusu nia ya al Mangoush ya kushirikiana kikamilifu na utawala haramu wa Israel ni ya uongo kabisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live