Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Libya: Waokoaji wanne kutoka Ugiriki wafariki katika ajali ya barabarani

Libya: Waokoaji Wanne Kutoka Ugiriki Wafariki Katika Ajali Ya Barabarani Libya: Waokoaji wanne kutoka Ugiriki wafariki katika ajali ya barabarani

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: Voa

Waziri wa Afya wa Libya amesema waokoaji wanne wa Ugiriki waliotumwa nchini Libya, kutoa usaidizi, kufuatia mafuriko makubwa katika mji wa mashariki wa Derna, walifariki katika ajali ya barabarani.

Takriban watu 11,300 walikufa wakati mabwawa mawili ya maji yalipovunja kingo, kufuatia dhoruba iliyopewa jina la Daniel wiki iliyopita, na kusababisha maji mengi zaidi kusomba watu na mali katika jiji hilo, kulingana na shirika la misaada la Red Crescent.

Watu wengine 10,000 hawajulikani walipo, na wanadhaniwa kuwa wamekufa. Siku ya Jumapili, basi lililokuwa limebeba waokoaji 19 wa Ugiriki liligongana na gari lililokuwa limewabeba raia watano wa Libya kwenye barabara kati ya miji ya Benghazi na Derna.

Raia watatu wa Libya waliokuwa kwenye gari hilo pia waliuawa. Mkasa huo wa mafuriko umeleta umoja adimu kwa Libya yenye utajiri wa mafuta, ambayo imegawanyika kati ya serikali hasimu za mashariki na magharibi mwa nchi hiyo, zinazoungwa mkono na vikosi mbalimbali vya wanamgambo na jumuiya za kimataifa.

Wakaazi kutoka miji ya karibu ya Benghazi na Tobruk wamejitolea kuwapa hifadhi waathiriwa, huku watu wengi wakijitolea kuwatafuta manusura waliofukiwa chini ya vifusi.

Chanzo: Voa