Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Libya:Tunaunga mkono ukombozi Palestina

Libya Palestina Libya:Tunaunga mkono ukombozi Palestina

Fri, 1 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya maandamano makubwa ya wananchi wa Libya kulaani kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo na Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala haramu wa Israel, Waziri Mkuu wa Libya amesema: Tripoli inaunga mkono suala la ukombozi wa Palestina.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Abdul Hamid al-Dbeibeh, Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya yenye makao yake Tripoli, Alhamisi jioni kwa mara nyingine alisisitiza uungaji mkono wa nchi hiyo kwa suala la Palestina na mapambano ya kupigania ukombozi Wapalestina dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Waziri Mkuu wa Libya pia amesema: Tunapinga kuanzisha uhusiano wowote na Israel.

Jumapili iliyopita vyombo vya habari vya Israel viliripoti kuhusu kikao cha siri kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Tel Aviv, Eli Cohen na Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya al-Manoqhosh huko Roma, Italia, kilichofanyika katika hatua ya kwanza kwa lengo la kujadili uhusiano kati ya utawala wa Kizayuni na Libya.

Baada ya kufichuliwa kwa mkutano huo na vyombo vya habari vya Kizayuni, maandamano mengi yalifanyika katika miji ya Libya kuupinga, ambapo waandamanaji walichoma moto bendera ya Israel na kufunga barabara za miji kadhaa ya Libya. Najla Al-Mangoush (kushoto) na Eli Cohen

Jumatatu iliyopita, al-Dbeibeh alimuondoa rasmi Najla Al-Mangoush kwenye nafasi yake.

Al-Mangoush alikiri kuwa alifanya mazungumzo na Eli Cohen kwa uratibu wa waziri wa mambo ya nje wa Italia, Antonio Tajani, lakini amedai kuwa mazungumzo hayo hayakuwa rasmi na kwamba hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa.

Inadokezwa kuwa Al Mangoush sasa amekimbilia Uturuki baada ya Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya kumsimamisha kazi.

Baadhi ya viongozi na wanasiasa mashuhuri wa Libya wametoa mwito wa kuondolewa mamlakani serikali nzima ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo baada ya kashfa hiyo ya mkutano wa Al Mangoush na Wazayui.

Khalid al-Mishri, Mwenyekiti wa zamani wa Baraza Kuu la Uongozi la Libya amelaani mkutano baina ya wawili hao ambao anasisitiza kuwa, yumkini si wa kwanza kufanyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live