Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Libya: Nchi iliyo katika mgogoro tangu kupinduliwa kwa Gaddafi

Libya: Nchi Iliyo Katika Mgogoro Tangu Kupinduliwa Kwa Gaddafi Libya: Nchi iliyo katika mgogoro tangu kupinduliwa kwa Gaddafi

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Libya imekuwa katika mgogoro tangu mtawala wa muda mrefu Kanali Muammar Gaddafi kupinduliwa na kuuawa mwaka 2011.

Tangu 2014, imegawanyika kisiasa kati ya serikali ya mpito inayotambuliwa kimataifa huko Tripoli (magharibi), na utawala wa Tobruk (mashariki) - ambao hauitambui serikali ya Tripoli.

Derna, ngome ya zamani ya Islamic State wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya Gaddafi, sasa inadhibitiwa zaidi na utawala wa mashariki.

Nchi ambazo zingependa kutuma usaidizi zina matatizo katika kufanya majadiliano na tawala hizo mbili.

Lakini licha ya mgawanyiko huo, serikali mjini Tripoli imetuma ndege yenye tani 14 za vifaa vya matibabu, mifuko ya mwili na zaidi ya madaktari 80 na wahudumu wa afya.

Chanzo: Bbc