Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Libya: Hati yatolewa kukamatwa maafisa waliohusika na mafuriko

Mafuriko Ya Libya: Kuna Harufu Kali Ya Maji Taka Na Kifo Libya: Hati yatolewa kukamatwa maafisa waliohusika na mafuriko

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Libya ametoa amri ya kukamatwa kwa maafisa wengine wanne kutoka jiji la Derna. ikiwa ni katika kuendelea na uchunguzi wake kuhusiana na kesi ya kuvunjika mabwawa yaliyosababisha mafuriko makubwa katika mji huo.

Kwa mujibu wa taarifa, wajumbe wawili wa Baraza la Manispaa ya Derna, mkurugenzi wa ofisi ya miradi ya ujenzi wa jiji na mkuu wa kamati ya kiufundi inayohusika na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jiji wamekamatwa kwa tuhuma za usimamizi mbaya na ubadhirifu wa fedha.

Hapo awali, shirika rasmi la habari la serikali ya Libya "WAL" liliripoti: kuwa Sadiq al-Soor", Mwanasheria Mkuu wa nchi hii, alitangaza mwanzoni mwa uchunguzi wake kuhusu maafa ya yaliyosababishwa kimbunga cha Daniel ikiwa ni pamoja na kuporomoka kwa mabwawa mawili katika jiji la Derna, ili kubaini iwapo maafa hayo yalitokana na rushwa au uzembe wa maafisa wa serikali.

Jumatatu wiki jana, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilitoa hati ya kukamatwa kwa maafisa wengine 16 wa Libya ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa kubomoka kwa mabwawa ya Wadi Derna na Abu Mansour baada ya mafuriko.

Tarehe 10 Septemba, kimbunga kikubwa ilikumba maeneo kadhaa nchini Libya na kusababisha uharibifu mkubwa mashariki mwa nchi hiyo, maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa na kutoweka.

Takwimu za hivi punde zilizochapishwa na vyanzo rasmi, mafuriko nchini Libya yamepelekea watu 4255 kupoteza maisha, na wengine zaidi 8540 bado hawajulikani walipo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, takriban watu 43,000 ni wamekuwa wakimbizi wanaishi katika kambi za wakimbizi. Hali baada ya mafuriko Libya

Wakati huo huo , Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) umetilia mkazo tena wajibu wa kudhaminiwa mahitaji ya kibinadamu katika maeneo ya mashariki mwa Libya kutokana na uharibifu mkubwa uliofanywa na mafuriko ya hivi karibuni.

Katika taarifa yake hiyo, UNSMIL imesema: "Suala la kudhaminiwa mahitaji ya kibinadamu linaendelea kuwa muhimu. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamegundua kuwa, nusu ya vituo vya afya 78 vilivyofanyiwa tathmini huko Derna na sehemu za Al-Jabar Al-Akhdar havifanyi kazi kwa kiasi fulani au havifanyi kazi kabisa. Mafuriko yameharibu pia mitandao ya maji safi, mabomba na mitaro ya maji taka."

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imesema kuwa, familia nyingi zilizopoteza makazi kutokana na mafuriko zinahifadhiwa maskulini huku serikali za mitaa zikifanya kazi kwa bidii kutafuta utatuzi wa changamoto zao nyingi zikiwemo za mahala pa kukaa. Vile vile imesisitizia haja ya kushughulikiwa haraka hali ya watu waliokimbia makazi yao na kutafuta hifadhi katika maeneo ya skuli, kabla ya kuanza mwaka mpya wa masomo.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameomba msaada wa dola milioni 71.4 za Kimarekani ili kukidhi mahitaji ya haraka ya watu 250,000 walioathiriwa vibaya zaidi, katika muda wa miezi mitatu ijayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live