Muungano wa mataifa ya ECOWAS, umeonya waliokuwa wagombea wa urais nchini Liberia dhidi ya kuanza kujitangaza washindi wakati huu tume ya uchaguzi ikiendelea na hesabu ya kura, ECOWAs ikisema hilo litachangia vurugu.
ECOWAS, imesema hatua yake imetokana na baadhi ya wagombea 19 walioshiriki kwenye kinyanganyiro cha urasi kuanza kudai wao ndio washindi ili hali tume ya chaguzi bado inaendelea na zoezi la hesabu kura ambalo linatarajiwa kukamilika kwa kipindi cha majuma mawili yajayo.
Ecowas katika onyo lake imesema itawachukulia hatua wanasiasa ambao watachochea vurugu baada ya uchaguzi ulioshuhudia utulivu nchini Liberia.
Duru ya pili ya uchaguzi itafanyika mapema mwezi ujao iwapo hapatakuwa na mgombea atakayefanikiwa kupata asilimia inayohitajika kutangazwa mshindi wa urais.
Uchaguzi huo wa Liberia ni kwanza kufanyika tangu tume ya umoja wa mataifa kukamilisha shughuli ya kulinda amani nchini humo mwaka 2019, ambayo iliundwa baada ya vita vya wenyewe kwa wenye vilivyosabisha zaidi ya watu alfu 250 kupoteza maisha.