Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liberia: Gari lagonga wafuasi wa mshindi wa urais, laua watu kadhaa

Liberia Gari Wafuasi Liberia: Gari lagonga wafuasi wa mshindi wa urais, laua watu kadhaa

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gari moja limevamia umati wa wafuasi wa mwanasiasa Joseph Boakai aliyeibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais huko Monrovia, na kuua watu wasiopungua wawili na kujeruhi wengine wengi.

Habari hiyo imethibitishwa na wahudumu wa hospitali, polisi na duru za kisiasa za Liberia.

Japokuwa maafisa wa polisi hawakutaka kuzungumzia chanzo cha mkasa huo, lakini msemaji wa chama cha Boakai amesema hana shaka kuwa shambulizi hilo limefanywa kwa makusudi.

Polisi wa Liberia wanasema dereva wa gari hilo aliyeua wafuasi wa mshindi wa kiti cha rais ametoweka.

Sia Wata Camanor, afisa katika Hospitali ya John F. Kennedy, hospitali kuu ya Monrovia, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba: "Watu wawili wamefariki dunia na mmoja yuko katika hali mbaya,". Ameongeza kuwa watu wengine ishirini wamejeruhiwa.

Tukio hilo lilijiri jioni ya jana baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutangaza rasmi ushindi mwembamba wa Joseph Boakai dhidi ya rais anayeondoka madarakani, George Weah, katika uchaguzi wa rais wa marudio wa tarehe 14 Novemba.

Uchaguzi huo uligubikwa na hofu ya kutokea ghasia baada ya kutangazwa matokeo, lakini washirika wa kigeni wa Libeŕia wamepongeza njia ya amani iliyotawala zoezi hilo katika nchi inayoendelea kupata ahueni baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoendelea kwa miaka mingi.

Rais anayeondoka wa Liberia, George Weah, amekiri kushindwa na mpinzani wake, Joseph Boakai, katika duru ya pili ya uchaguzi mkuu wa urais baada ya kinyang'anyiro kikali. George Weah

Nyota huyo wa zamani wa soka, ambaye amewahi kutwaa tuuzo ya mchezaji bora wa dunia, amesema ni wakati wa kuweka mbele maslahi ya Liberia badala ya maslahi binafsi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live