Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

LIBYA: Uchunguzi wa UN wafichua jinsi watu walivyozikwa kwa pamoja jangwani

UN LIBY A MAKABURI Uchunguzi wa UN wafichua jinsi watu walivyozikwa kwa pamoja jangwani

Wed, 6 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jopo la Umoja wa Mataifa nchini Libya limetangaza habari ya kugundua 'makaburi ya umati' ambayo hayajafanyiwa uchunguzi, huku likiitaka Tripoli ifanye upekuzi zaidi na kuyachunguza makaburi yaliyogunduliwa.

Jopo hilo linatazamiwa wiki hii kulikabidhi Baraza la Haki za Binadamu la UN ripoti kuhusu makaburi hayo mapya ya umati yaliyogunduliwa katika mji wa Tarhauna, magharibi mwa Libya. Jopo hilo la Umoja wa Mataifa nchini Libya limebainisha kuwa, yumkini makaburi hayo ya umati yanapindukia 100.

Limeeleza namna genge la wanamgambo lililokuwa likiongozwa na ndugu saba liliua na kuwazuilia mamia ya watu kati ya mwaka 2016-2020 katika mji huo.

Jopo hilo la UN limesema genge hilo lilikuwa likiwatesa na kuwakandamiza watu waliokuwa wakishikiliwa na kundi hilo katika jela zao, baadhi wakiwekwa kwenye kijisanduku kinachofanana na tanuri, na kisha kuwachoma moto wakati wa kuwasaili.

Mji wa Tarhauna ulioko yapata kilomita 90 kusini mwa mji mkuu Tripoli, ulikuwa ngome ya vikosi vya Jenerali muasi Khalifa Haftar wakati wa kampeni zao za kutaka kuiteka Tripoli, mji mkuu wa Libya.

Libya imeathiriwa na machafuko na uksoefu wa amani tangu kupinduliwa kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011 kwa uingliaji wa nchi ajinabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live