Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa nini Hujampeleka Kwa Wazazi: Moses Kuria atania Rais Uhuru kuhusu Raila

1f9381e14cbb6e91 Kwa nini Hujampeleka Kwa Wazazi: Moses Kuria atania Rais Uhuru kuhusu Raila

Mon, 10 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Kuria anasema Raila anachezwa kisiasa kupitia mkataba wa handisheki kati yake na Rais

- Alihoji ni kwa nini Rais hajawahi kumtembeza nyumbani kwake Mt Kenya hata siku moja iwapo kweli kuna ndoa kati yao

- Baadhi ya wanaODM pia wamekuwa wakiibua wasiwasi kuwa Raila anatumika kisiasa na kisha atatemwa na Rais

- Suala sugu ni kuhusu maeneo bunge mapya 70 yaliyopendekezwa na BBI mabadiliko ya katiba yakifanywa

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria ametania uhusiano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.

Kenyatta na Raila waliingia kwenye ndoa ya kisiasa Machi 9 2018 kupitia mkataba wa handisheki ambapo walitangaza kumaliza uhasama wa kisiasa baina yao.

Ni ndoa ambayo ilileta migogoro ndani ya Jubilee kiwango cha kuibua mirengo kati ya wanaomuunga mkono Rais na wale wanaoegemea upande wa naibu wake William Ruto.

Kuria hata hivyo alitumia ukurasa wake wa Facebook kutilia shaka uhalali wa ndoa hiyo kwani bado mke hajatambulishwa kwa wazazi.

Kuria alisema hakuna ndume ambaye anaweza kukaa na binti kwa kipindi hicho bila kumtambulisha kwa wazazi wake.

"Na huyu bibi tangu Machi 2018 mbona haujampeleka kwa wazazi Central? Kuria alimuuliza Rais Uhuru Kenyatta.

Ujumbe wa mbunge huyo ulijiri wakati ambapo baadhi ya wandani wa Raila wameibua maswali kuhusu handisheki na matunda yake.

Wakiongozwa na Seneta James Orengo na Mbunge Otiende Amollo wandani hao wa Baba wanasema lengo la handisheki ni kumtumia kisiasa.

Wawili hao wanasema maafisa wachache wa chama wanampotosha Raila kuhusu kuendelea kuunga mkono BBI kupitia kwa handisheki ilhali anachezwa karata.

Wamesema lengo ni kusaidia Mt Kenya kupata minofu zaidi kupitia mabadiliko ya kikatiba na kisha baadaye Rais Uhuru atamtema Raila.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari kemekem za TUKO hapa

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke