Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kutana na mume wa Jaji Mkuu mteule Martha Koome

D65a59ba9731d863 Kutana na mume wa Jaji Mkuu mteule Martha Koome

Fri, 30 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Hadi Machi 2021, mumewe Koome Kiragu aliwahi kuwa mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi kwa ajili ya Ubinadamu-Kenya (Habitat for Humanity-Kenya)

- Katika jukumu lake, aliongoza mipango anuwai ya kusaidia jamii zinazohitaji kukuza makazi bora na kuboresha matumizi ya maji, usafi wa mazingira, upatikanaji wa nishati na umiliki wa ardhi

- Mnamo 2018, alipata ufadhili wa KSh96 milioni kusaidia familia 120 kujenga nyumba za bei rahisi KSh 800,000 kwa kila nyumba kwa kushirikiana na Serikali ya Kaunti ya Homa Bay.

Uteuzi wa Jaji Martha Koome kujaza nafasi ya Jaji Mkuu umealika udadisi mwingi kuhusu maisha yake ya kikazi na ya kibinafsi.

Wakati akihojiana kwa wadhifa huo, Jaji Koome alisema kuwa ameolewa na ana watoto watatu.

Hadi Machi 2021, mumewe Koome Kiragu aliwahi kuwa mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi kwa ajili ya Ubinadamu-Kenya (Habitat for Humanity-Kenya).

Shirika hilo ni sehemu ya harakati ya ulimwengu ambayo inataka kuwezesha watu walio katika mazingira magumu kupata makazi bora na kuimarisha ubora wa maisha yao.

Katika jukumu lake, aliongoza mipango anuwai ya kusaidia jamii zinazohitaji kukuza makazi bora na kuboresha matumizi ya maji, usafi wa mazingira, upatikanaji wa nishati na umiliki wa ardhi.

Kiragu alishirikiana na taasisi zingine mfano benki na mashirika ya serikali kutoa makazi bora kwa jamii za Wakenya.

Mnamo 2018, alipata ufadhili wa KSh96 milioni kusaidia familia 120 kujenga nyumba za bei rahisi KSh 800,000 kwa kila nyumba kwa kushirikiana na Serikali ya Kaunti ya Homa Bay.

Mapema mwaka huu, Kiragu alishirikiana na benki ya eneo hilo kujenga nyumba za wakimbizi wa ndani wanaoishi Mai Mahiu.

Alikuwa amefanya kazi na familia zaidi ya 300 ambazo ziliweza kukusanya pesa na kununua ardhi kwa makazi mapya.

Mbali na nyumba za makazi, Kiragu pia alisaidia kujenga shule katika maeneo tofauti ya kaunti na alitambuliwa kuwa shujaa wa kaunti na Serikali ya Kaunti ya Laikipia.

Aliweka msingi bora katika NGO na aliwahi kuwa mwanachama wa bodi ya kimataifa ya shirika na alichaguliwa kwa bodi ya uongozi, ambayo ilimfanya kuwa Mwafrika pekee katika shirika hilo.

Baadhi ya majukumu yake yalimtaka kusafiri nje ya nchi na Jaji Koome angeandamana naye katika safari zingine.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690. Tazama habari zaidi hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke