Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kusimamishwa kwa Shughuli za kisiasa Mali, Mahakama yabaki na kigugumizi

Maliiiiii Kusimamishwa kwa Shughuli za kisiasa Mali, Mahakama yabaki na kigugumizi

Sun, 28 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Katiba nchini Mali imetangaza kuwa haina uwezo kuchunguza malalamiko ya kutaka kubatilishwa uamuzi uliochukuliwa na Serikali ya Kijeshi kusimamisha shughuli za kisiasa.

Katika maamuzi mengine, Mahakama ilitangaza kuwa haikubali au kupokea maombi mbali mbali kutoka kwa Mashirika ya Mahakimu na waendesha mashtaka kuhusu kuvitetea vyama hivyo vya kisiasa nchini Mali.

Hivi karibuni nchi ya Mali ilitangaza kusimamisha shuguli zote za kisiasa na kupiga marufuku vyombo vya habari kutangaza shughuli zao.

Vyama hivyo vinashutumiwa katika kuleta majadiliano hasi na upotoshaji vitu vinavyoweza kuathiri usalama wa nchi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live