Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kupotea kwa umeme Kenya kwachochea hasira ya umma

Kupotea Kwa Umeme Kenya Kwachochea Hasira Ya Umma Kupotea kwa umeme Kenya kwachochea hasira ya umma

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Wakenya wanataka majibu baada ya huduma za umeme kukatizwa nchini kote usiku wa Jumapili.

Taifa hilo la Afrika Mashariki lilitumbukia gizani mwendo wa saa mbili kwa mara ya tatu katika kipindi cha miezi minne iliyopita.

Hitilafu hiyo ilitatiza huduma kadhaa, ikiwa ni pamoja na katika uwanja mkuu wa ndege katika mji mkuu, Nairobi, ambapo vituo viwili vilikosa umeme kwa saa kadhaa.

Wakenya wanaikosoa serikali, huku hasira zikiongezeka kutokana na hali ya umeme kupotea mara kwa mara.

Kufikia Jumatatu asubuhi, umeme ulikuwa umerejeshwa sehemu kubwa ya nchi, isipokuwa katika baadhi ya maeneo ya Nairobi na eneo la Pwani.

"Tunafanya kazi usiku na mchana kurejesha hali ya kawaida katika maeneo yaliyosalia haraka iwezekanavyo," Kenya Power, shirika la serikali linalotoa huduma wa umeme lilisema katika sasisho katika taarifa.

Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen amebeba mzigo mkubwa wa ukosoaji huo.

"Kenya Power inapaswa kutoa fidia ya kifedha kwa hasara ya umeme kupotea.Ni wakati wa Kenya Power kuwajibika kwa kukatika kwa umeme," Mkenya mmoja alisema kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Bw Murkomen amekosolewa kwa kuruhusu kukatika tena kwa umeme katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), licha ya kutoa ahadi mnamo Agosti - wakati Kenya ilikabiliwa na hitilafu ya muda mrefu zaidi ya umeme nchini kote katika miaka ya hivi majuzi - kwamba kukatika kwa umeme katika uwanja huo ‘hakungetokea tena".

Chanzo: Bbc